Kama ulikua hujui Telstar 18 ndio mpira utakao tumika katika fainali za kumbe dunia nchini Russia

Kwa kuwa kila fainali za Kombe la Dunia zina mpira maalum, inaonekana kutakuwa na uchunguzi wa mpira wa fainali za mwaka huu, ambao tayari kampuni ya Adidas imeshaundaa kwa ajili ya mashindano hayo ya Fifa yanayofanyika kila baada ya miaka minne tangu mwaka 1970.

Tayari mpira wa mwaka huu, ambao unaitwa Telstar 18, umeshakosolewa na baadhi ya makipa kuwa unapaa na mgumu kuukamata.

Lakini wanasayansi wanasema mpira huo mpya ni imara pengine kuliko Jabulani, mpira wa fainali za Kombe la Dunia zilizofanyika Afrika Kusini mwaka 2010 ambao ulikosolewa sana.

Telstar 18 unafanana na mpira wa kwanza wa Adidas wa fainali za Kombe la Dunia ulioitwa Telstar ambao ulitumiwa nchini Mexico mwaka 1970.

Huo ulikuwa mpira wa kwanza wa rangi nyeusi na nyeupe uliotengenezwa kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia ulibuniwa ili uonekane vizuri zaidi kwenye televisheni zisizo za rangi na unajulikana kwa kuwa na mchanganyiko wa vipande vya pembe tano na sita ambavyo vimefanya soka sasa itambuliwe kwa kutumia alama ya mpira huo.

Mpira utakaotumika Russia ni wa rangi nyeupe, nyeusi na kijivu, huku kukiwa na michirizi ya rangi ya dhahabu.

Eric Goff, profesa wa fizikia katika Chuo Kikuu cha Lynchburg cha Virginia, alikuwa mmoja wa jopo lililochambua mpira huo kwa kuupitisha kwenye sehemu ya upepo na ardhini.

Kwa kulinganisha na Brazuca, mpira uliotumika Brazil mwaka 2014, Telstar 18 ulionekana kutokata upepo wakati ukipaa, watafiti walibaini.

Hii inamaanisha kuwa mpira huo hausafiri kwenda mbali yaani unaenda asilimia nane hadi kumi chini ya kiwango cha Brazuca — wwakati unapopigwa kiki kali ya kasi ya kilomita 90 kwa saa, Goff aliiambia AFP.

“Hiyo inaweza kuwa habari mbaya kwa washambuliaji ambao hupenda kupiga mashuti ya mbali na hivyo hawana budi kupiga mpira kwa nguvu zaidi,” alisema.

Lakini pia habari nzuri kwa makipa, kwa kuwa mpira ukipigwa kwa kasi, utawafikia ukiwa umepunguza kasi kuliko ilivyokuwa kwa Brazuca mwaka 2014.”

Kama Brazuca, Telstar 18 una vipande sita, kulinganisha na nane vya Jabulani– ikiwa ni vichache sana kuliko mpira asilia wenye vipande 32.

Lakini vipande vya Telstar 18 vina umbile tofauti, na uzi unaoviunganisha ni mrefu asilimia 30 kuliko Brazuca, ingawa pia ni mwembamba.

Sungchan Hong wa Chuo kikuu cha Tsukuba, kitivo cha sayansi ya michezo nchini Japan, alisema majaribio ya kupiga mpira huo kwa kutumia yalibainisha kuwa “Telstar 18 una tao imara la mtupo hewani kuliko mipira ya awali”.

“Kwa maneno mengine, mipira ya adhabu kama za moja kwa moja au kona, au mashuti ya umbali wa kati inaweza kuwa na ufanisi,” aliiambia AFP.

“Sidhani kuwa kutakuwa na kiwango kikubwa cha mienendo isiyotarajiwa” kama Jabulani ulivyokuwa, aliongeza Hong. “Sidhani kama makipa watapaathirika.”

Kwa kulinganisha na Jabulani, Telstar 18 itaonyesha mwenendo wa kutua usipotarajiwa kama mpira wa baseball, ambao huyumba hewani.