Jamii imetakiwa kuwachunguza walimu wa Madrasa kabla ya kuwakabidhi watoto

Jamii imetakiwa kuwachunguza walimu wa Madrasa kabla ya kuwakabidhi watoto kuwafundisha ili kuwakinga na Vitendo viovu vilivyo enea katika jamii ya Zanzibar.

Hayo yamesemwa na Naibu Kadhi wa Zanzibar Hassan Othman Ngwali katika hafla ya Mashindano ya Qur an yaliyofanyika Masjid Muhamad Mwanakwerekwe Mkoa wa Mjini Magharib Unguja yaliyo andaliwa na Direct Aid.

Moja ya washiriki katika Mashindano hayo ndugu Omar Ali Ahmad
yaliyoandaliwa na Direct Aid ya juzuu 30.

Shekhe Othman Ngwali amewataka walimu wa Madrasa kuhakikisha wanajenga uaminifu kwa wazazipale wanapo kabidiwa watoto na wasiwe chanzo cha kuwatendea vitendo viovu.

Kwa upande mwengine amesisitiza suala la jamii kukisoma kitabu cha Allah (Qur an) ili kujiepusha na maovu na kupata malipo ya thawabu kesho Akhera (Kiyama).

Aidha ameusi waislamu kuzidisha ibada katika kumi hili la mwisho na kuswali swala za usiku ambazo zitawajenga kuwa wachamungu na kuiga sifa ya Mtume Muhamad (S.W).

Kwa upande wake mkuregenzi wa Shirika hilo la Direct Aid Aiman Kamal Din amesema Mashindano hayo yamepewa jina la muasisi wa Shirika Hilo Direct Aid Abrahaman Sumait ili kumtakia dua kiongozi huyo ambaye
ameshafariki dunia muda mrefu.

Naibu kadhi Zanzibar Othman Ngwali akambidhi zawadi Nasra Muhamed
katika hafla iliyofanyika Msikiti wa Masjid Muhamd Kwerekwe.

Aidha ametoa shukrani kwa Ofisi ya Mufti Zanzibar kwa kuwaunga mkono katika jitihada zao za kuisadia jamii ya Zanzibar kwa kujenga msikiti,kuchimba visima na shughuli nyengine za kijamii na Mashindano
hayo yatakuwa na muendelezo.

Jumla ya washiriki 26 wameshiriki katika Mashindano hayo ya kwanza jumla ya washiriki 10 kutoka Pemba na 16 kutoka Unguja.

Kwa upande wa washindi wa Mashindano hayo mshindi wa kwanza Nassir Rashid Seif amepata alama 100, Omar Ali Ahmad amepata alama 99.95, mshindi wa tatu Nasra Muhamed Juma amepata alama 99.8 kwa upande wa mshindi wa nne Haji Jumbe Haji amepata alama 99.8 na mshindi wa Tano Ibrahim Ali Khatib amepata alama 99.

Mashindano hayo yalikuwa kwa njia ya Tilawat kwa juzuu 30  kwa Wanawake na wanaume chini ya umri wa miaka 20.

 

Ibrahim makame