Kujiuzulu kwa Rais Ravia kwaishangaza ZFA

Chama cha mpira Miguu Zanzibar (ZFA) kimesema kimeshtushwa na kitendo cha Raisi wa chama cha mpira wa miguu Zanzibar kujiuzulu bila ya kutaja sababu ya msingi kwenye barua yake aliyoituma kwenda ZFA.

Akizugumza na Zanzibar24 Katibu Mkuu wa chama hicho Muhamed Ali Hilali amesema  licha ya Raisi Ravia kuleta barua hiyo bila ya sababu ya msingi inafanya ZFA kupigwa na mshangao .

Aidha ameeleza wao kama ZFA wameipokea barua hiyo ingawa imeiweka tasisi hiyo katika kipindi kigumu, hata hivyo ameeleza ZFA haijakaa kikao hata kimoja kiijadili barua ya  Ravia Idarous.

Kuhusu nani atarisi nafasi hiyo Muhamed Hilali amesema kwa mujibu wa Katiba ya ZFA makomo wa Raisi Pemba Ali Muhamed ndie atakae chukua nafasi ya Uraisi wa ZFA kwa sasa licha nae yupo katika zengwe la kujiuzulu.

“Tutaharikisha kikao cha kamati tendaji haraka sana ili kijadili suala hili kwa pande zote mbili Unguja na Pemba “alisema Muhamed Hilali.

Kwa upande mwengine Hilali amezugumzia suala linalo semwa kwa Zanzibar kufungiwa mwaka mmoja na CECAFA si kweli suala hilo limeshamaliza muda mrefu.

“Haya mambo yameisha ya CECAFA Musonye amekiuka taratibu za utawala kumtumia Mzee Zamu barua pepe kwenye anuani yake binafsi” Alifahamisha Hilali.

Aidha ameeleza wameshapokea ratiba ya Mashindano ya Kagame Cup, CECAFA ya Wanawake Rwanda na soka la Ufekweni nchini Uganda.