Raisi wa mchezo wa Kick Boxing Zanzibar ameitaka S M Z kuunga mkono mchezo huo

Raisi wa mchezo wa Kick Boxing Zanzibar ambaye amewahi kuwa Bingwa wa Mashindano mbali mbali Ashraf Suleiman ameitaka serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuunga mkono mchezo huo ambao utaitangaza Zanzibar kimataifa.

Akizugumza na Zanzibar24 nyumabani kwake Mpendae  Ashraf amesema yeye binafsi ameteuliwa na Shirikisho la mchezo Kick Boxing duniani ( WKNY) kuwa Raisi wa Chama cha mchezo huo kwa upande wa Zanzibar ambao inapeperusha bendera kama Zanzibar.

Aidha Ashraf amefunguka na kusema kuwa yeye binafsi bado ameshakilia mataji mengi ambayo Mpaka leo hajapakonywa na mtu yeyote Mpaka leo na historia nayo duniani kama mzanzibari kwa miaka sita sasa.

“Tuliwahi kufika Baraza la Michezo Zanzibar mimi na raisi wa WKNY kunitambulisha kama mimi ndie Raisi baada ya kushinda mchezo wa dunia Kick Boxing” Alifahamisha Ashraf Sleman.

Kuhusu michezo ya kimataifa  amefunguka na kusema tayari wameshapewa Mashindano ya kimataifa kama Zanzibar kusafiri nje ya nchi kwenye Mashindano mbali mbali kama vile ya Uingreza kwenda kugombania taji jengine mwezi saba tarehe 30.

“ Tarehe 28 mwezi ujao vijana wangu wanatarajia kwenda France kwenye kisiwa cha Mayole Mashindano yanayoitwa Kick Boxing Title mabondia kutoka Zanzibar watashiriki wanne Nassor Sindano kg 72, Bandago kg 77 na Viroba kg 79” Alifahamisha Ashraf Sleman.

Aidha Ashraf amewataka wadau kujitokeza kuunga mkono mchezo huo kwani ndio unaotangaza utalii wa Zanzibar hususan yeye anaposafiri kuwatangaza wazanzibari kwenye sekta ya utalii inakuwa na uchumi unakuwa kwa Zanzibar.

Jumla ya vijana 30 anawafundisha kwenye eneo lake la mazoezi kila siku ili kutengeza wanamichezo hao na kuukuza mchezo huo kwa ujumla ili jumla ya vijana nane tayari wameshafikia kiwango cha upiginaji kimataifa.