Walimu wanaofanya vitendo vya udhalilishaji mashuleni kuchukuliwa hatua – Waziri Ndalichako

Serikali kupitia Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako imesema haiwezi kuvumilia vitendo vya udhalilishaji ambavyo vimefanywa na mwalimu wa shule St. Florence iliyopo jijini Dar es salaam.

Ndalichako ameyasema hayo wakati akikabidhi zawadi kwa shule na wanafunzi wa darasa la saba, kidato cha nne na sita jijini Dodoma baada ya kufanya vizuri kwenye matokeo ya mwisho ya mitihani yao

“Nitumie nafasi hii kukemea vikali vitendo vya udhalilishaji vinavyofanywa na baadhi ya walimu katika shule zetu tumeshududia shule ya S.t Florence ambayo mwalimu anafanya vitendo vya udhalilishaji serikali haiwezi ikavumilia vitendo vya namna hiyo na pia serikali haiwezi kuvumilia kuwa na shule ambazo haziwahakikishii watoto usalama wao, unajiuliza katika akili ya kawaida yani shule inampangia mwalimu wa kiume kuwasindikiza mabinti kuna taratibu zetu za kulea watoto,” alisema Ndalichako.

“Kwahiyo ni jukumu la serikali watoto wanapokuwa shuleni na niwahakikishie Watanzania kwa ujumla kwamba serikali itahakikisha kwa yoyote yule anayefanya vitendo vya kuwadhalilisha watoto shuleni serikali itachukua hatua kali nataka niwahakikishie Watanzania wale waliokuwa wanafanya vitendo vya udhalilishaji s.t Florence vyombo vya dola vinafuatilia na baada ya uchunguzi serikali itasema hatua ambazo zitachukuliwa lakini niwahkikishie kwamba zitakuwa ni hatua kali.”

Hivi karibuni kulitokea sintofahamu Tanzaniabaada ya kuwepo na taarifa kwamba katika shule ya St. Florence mwalimu mmoja aliyetajwa kwa jina la Ayubu kudaiwa kuwanajisi watoto wanne wa darasa la saba.