Ombaomba huondoa haiba ya mji – RC Ayoub

Mkuu wa mkoa wa mjini Ayoub amesema  Serikali  ya  mkoa wa mjini kwa kushirikiana  na  serikali  ya mkoa wa Dar es salam  imekusudia  kushirikiana  katika  kuwaondosha  ombaomba wanaotoka  Tanzania  bara  kuwarejesha  kwao  na wale wa Zanzibar  kuondosha  na kurudishwa  kwenye  makaazi yao ili kuuweka  mji  katika  taswira  na mandhari  ya  kuvutia.
Akizungumza na waandishi  wa habari  huko ofisin kwake  amesema uwepo wa ombaomba katika mandhari  ya  mji  inaondoka  haiba na uzuri wa mji  hivyo serikali hizo zitahakikisha  linadhibiti ombaomba katika maeneo hayo.
Wakati huo huo amezungumzia tatizo la  ubovu  wa  barabara  unaowakabili  wananchi  wa  kinuni  Mkuu huyo amesema kutokana na kuwepo tatizo  hilo serikali  inatafuta kila  njia kuhakikisha  inalipatia  ufumbuzi tatizo hilo  linalowapa  usumbufu wakaazi wa huko.