Trump na Kim Jong-un wawasili Singapore

Rais wa Marekani Donald Trump na Kiongozi wa Korea Kaskazini, Kim Jong-un wamewasili Singapore kwa ajili ya mkutano wao unaoelezwa kuwa wa kihistoria.

Trump aliwasili saa chache tu baada ya Kim kuwasili na ujumbe wake.

Mkutano wao ambao ni wa kwanza utafanyika siku ya Jumanne katika kisiwa cha Sentosa.

Mkutano

Rais Trump amesema ana furaha sana kuwa Singapore kwa mkutano huo.

Vyombo vya habari vya serikali Korea Kaskazini navyo vimesema mazungumzo hayo yanatoa fursa ya kuwepo kwa uhusiano mpya kati ya taifa hilo na Marekani.

Marekani ina matumaini kuwa kukutana kwao utakuwa mwanzo wa mchakato ambao hatimaye itashuhudiwa Kim akiachana na mpango wake wa silaha za nyuklia.

Kim Jong-un aliwasili kabla ya Donald TrumpKim Jong-un aliwasili kabla ya Donald Trump

Uhusiano wa viongozi hawa wawili umepitia kwenye milima na mbonde kwa kipindi cha miezi 18 iliyopita, wakirushiana matusi na kutishiana vita kabla ya uhusiano wao kuchukua mkondo mwingine na kuamua wawili hao kukutana.