ACT-Wazalendo waandaa mjadala uchambuzi wa bajeti kuu

Chama cha ACT-wazalendo kimeandaa mjadala wa uchambuzi wa bajeti utakaowahusisha wahariri wa vyombo vya habari na wabobezi wa masuala ya uchumi.

Akizungumza leo  Juni 12, Katibu wa Itikadi,Uenezi na mawasiliano ya umma wa chama hicho, Ado Shaibu amesema mjadala huo utakuwa kwa mtindo wa mazungumzo na chai.

Katibu wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi Act Wazalendo, Ado Shaibu

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk Philip Mpango Alhamis ijayo atasoma bajeti kuu kwa mwaka 2018/19.

Shaibu amesema baada ya kusomwa kwa bajeti kuu, chama hicho kitafanya uchambuzi siku ya Jumapili Julai 17.

Amesema mbali na wahariri, watakuwa na taasisi kama Sikika, (inayojihusisha na afya), TGNP (masuala ya jinsia) na Haki Elimu(inayohusika na masuala ya elimu)

Amesema mwaka jana waliandaa kongamano la kuchambua bajeti lakini walizuiwa na polisi.

“Ndiyo maana tumeamua mwaka huu kufanya kwa mtindo wa breakfast talk (mazungumzo na chai).” amesema.