Mchango wa Rais Magufuli ujenzi wa msikiti mkuu Dar es Salaam

RAIS John Magufuli ametoa pesa taslim kiasi cha Tsh. Milioni 10 kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa mifuko 600 ya sementi itakayosaidi kwenye ujenzi wa Msikiti Mkuu wa BAKWATA unaoendelea kujengwa Kinondoni Jijini Dar es Salaam.

Rais ametoa mchango huo leo Juni 12, 2018 wakati akikagua maendeleo ya ujenzi wa Msikiti huo unaojengwa kwa ufadhili wa Mfalme wa Morocco.

Msikiti huo ambao utakuwa mkubwa kuliko misikiti yote nchini Tanzania utabeba zaidi ya watu 8,000 na unatarajiwa kukamilika mwezi Aprili au mei mwakani.

“Napenda kuwaahidi viongozi wa dini zote kwamba serikali yangu itaendelea kushirikiana na dini zote,” amesema Rais Magufuli