SMZ yaendelea kutunza kazi za wasanii wakongwe Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia wizara ya Sanaa, Vijana na michezo imesema itandelea kulinda kazi za wasanii wakongwe na wapya ili zisitumike kiholela na watu wengine na kujipatia fedha .

Akijibu Swali la Mwakilishi wa Chake Chake Sleman Sarahan Saidi Naibu Waziri wa Sanaa, Vijana,Michezo Lulu Msham katika kikao cha Baraza la wakilishi ,ndugu Sleman Sarhan alitaka kujua wizara imejipanga vipi kulinda haki za wasanii na kutaka kujua je ipo sheria ya kulinda haki za wasanii Zanzibar.

Waziri Lulu Msham amesema wizara inatambua hilo ndio maan ikaamua kuunda kitengo cha hakimiliki za wasanii Zanzibar,

Aidha ameelezea mbinu zinatumika kuwasaidia wasanii wa Zanzibar ni kutoa elimu ya hakimiliki kwa jamii kupitia vipindi vya TV na Radio.

Amesema kuwa wasanii hao hupatiwa mirabaa kila mwaka kwa wasanii waliosajiliwa ikiwemo watunzi, watia mziki,wabunifu na kikundi kila mmoja hupewa asilimia 25%  kila mmoja ya mauzo ya kazi yao.

Aidha kwa upande wa Sheria ya kuwalinda wasanii Naibu waziri Lulu Msham amefafanua kuwa sheria hiyo ipo ya kudai haki za wasanii inayosimamia haki za Sanaa na Ulinzi kwa wasanii namba 14 ya mwaka 2013.

Akiuliza swali la nyongeza kupitia swala hilo la Msingi Sleman Sarhan ametaka kujua je kuna msanii mkongwe aliefaidika na haki miliki zake na (b) alitaka kujua utaratibu wa kufuata wasanii wakongwe au ambao wameshafariki kwenye familia zao ili kujua kudai haki zao.

Akijibu swali hili la nyongeza Naibu wa Ziri wa Sanaa,Vijana ,Utamaduni na Michezo amesema wapo wasanii wengi wanaendelea kufaidika ambao ni wagonjwa akimtaja Bi Mwema (Bi njiwa) miongoni mwa wasanii wakongwe wanao faidika na  wana utaratibu wa kuwajulia hali kama wizara.

Na: Ibrahim Makame.