Wazazi wahimizwa kuwapatia watoto wao haki zao za msingi

Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imewataka wazazi na walezi  nchini  kutekeleza majukumu yao ipasavyo pamoja na kuwapatia watoto haki zao za msingi.

Hayo yamebainishwa na waziri wa kazi, uwezeshaji, wazee, wanawake na watoto zanzibar Bi Muudline Cyrus Castiko wakati akitoa taarifa maaalumu kwa waandishi  wa habari  juu ya siku ya kupamabana na ajira za watoto.

Amesema ajira za watoto ni jambo linalodhofisha watoto na jamii kwa kiasi kikubwa ambapo kwa Zanzibar vitendo hivyo vimekuwa vikiongezeka kila siku kwa baadhi ya maeneo ambapo watoto huathirika kimwili, kiafya pamoja na kuwakosesha haki zao za msingi.

Wazir castiko alisema Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar imefanya jitihada mbali mbali kuhakikisha wanaondoa suala zima la  ajira za watoto ambapo kwa   utafiti uliofanywa na mtakwimu mkuu wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar wa mwaka 2014 umeonesha kuwa jumla ya watoto 25,803 wapo katika ajira za watoto sawa na asilimia 5.6 ya watoto walio chini ya umri kati ya miaka 5 hadi 17 na sawa na asilimia 47.3 ya watoto wate walioajiriwa na kuajiri.

Katika utafiti huo unaonesha watoto wa kiume walioajiriwa ni 15,885 na wa kike ni 9,948 pia amesema watoto wenye miaka 5-11 waliojiajiri sawa n asilimia 43.8 kati yao wanawake asilimia 49.4 na watoto wa kiume 40.2

Aidha amesema kutokana na takwimu hizo zanzibar inaungana na mashirika ya umoja wa mataifa kuadhimisha siku hii ya kupinga ajira za watoto.

Kila ifikapo tarehe 12 mwezi wa 6 dunia huadhimisha siku ya kupambana na ajira za watoto ikiwa na lengo la kuwapatia haki watoto ambapo kwa mwaka huu Taifa lililo salama na afya (generertion safety and helthy).

fathia shehe.