Mwanamme atafunwa na kichwa cha nyoka aliyekufa

Mwanamume mmoja katika jimbo ya Texas, Marekani ameponea chupuchupu kufariki baada ya kuumwa na kichwa cha nyoka ambaye alikuwa amemkata na kumuua.

Mwanamume huyo, alikuwa akifanya kazi shambani na alipomuona nyoka huyo wa urefu wa futi nne (1.25m) na alimkata kichwa kwa panga.

Alipouchukua mzoga wa nyoka huyo akautupe, kichwa cha nyoka huyo kilimuuma.

Ililazimu madaktari kumdunga sindano ya vipimo 26 vya dawa ya kuua sumu kumuokoa.