Nafasi za kazi wizara ya biashara viwanda na masoko Zanzibar

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi katika Wizara ya Biashara, Viwanda na Masoko kwa ajili ya Ofisi ya Wakala wa Kusimamia Viwanda Vidogo Vidogo na vya Kati (SMIDA) kama ifuatavyo:-

1.Afisa Mipango Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Mipango au Uchumi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2.Afisa Utawala Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Utawala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

3.Afisa Sheria Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya Sheria kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

4.Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Kutunza Kumbukumbu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5.Afisa Tehama Daraja la II “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya IT kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

6.Karani Mapokezi Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu elimu ya Sekondari na kufaulu.

7.Dereva Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Elimu ya Sekondari na awe amepata Leseni ya Udereva.
•Awe amepata mafunzo ya Udereva kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

8.Katibu Muhtasi Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Ukatibu Muhtasi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

9.Afisa Biashara Daraja la II “Nafasi 2”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Shahada ya Kwanza katika fani ya ‘Biashara’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

10.Afisa Manunuzi Msaidizi Daraja la III “Nafasi 1”

Sifa za Waombaji:
•Awe ni Mzanzibari.
•Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Ununuzi kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar

Jinsi ya Kuomba:
•Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-

KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 – ZANZIBAR.

•Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) N.B: Atakaewasilisha ‘Statement of Result’ au ‘Progressive Report’ maombi yake hayatazingatiwa.
g)Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 26 Juni, 2018 wakati wa saa za kazi.