Bodigadi wa Diamond Platinumz apata ajali, apasuka kichwa

Bodigadi wa Staa wa Bongo Fleva, Diamond Platinumz, Mwarabu Fighter amedai kuwa amepata ajali mbaya iliyosababisha kupasuka kichwani na kukimbizwa katika Hospitali ya Lugalo iliyopo Mwenge jijini Dar es Salaam kwa ajili ya huduma ya kwanza kabla ya kupelekwa Muhimbili kwa matibabu zaidi.

Mwarabu kupitia akaunti yake ya Instagrama amewashukuru madaktari wa Lugalo kwa huduma ya kwanza lakini hakueleza ajali hiyo imetokea lini, wapi na ilikuwaje.

Nduguzangu nimepata ajali mbaya sana nimepasuka kichwani ila nnawashukuru lugalo hosptal kwakunipatia uduma ya kwanza sasaiv wananikimbiza muhimbili kwaiyo dua zenu nduguzangu