Manispaa Ilala yazifungia maabara bubu na maduka ya dawa

Manispaa  ya Ilala imezifungia Maabara bubu na Maduka ya dawa yasio na sifa ambayo yanatoa huduma kinyume cha sheria.

Oparesheni hiyo endelevu ya kuzifungia Maabara hizo na maduka ya dawa imeanza Dar es Salaam  katika Jimbo  la Segerea , Ukonga  na Ilala.

Akizungumza na Waandishi wa Habari katika Operesheni hiyo  Mratibu wa Vituo Binafsi Manispaa ya Ilala Dkt. Wille  Sangu  amesema Maduka ya dawa ambayo wameyafungia ni yale  ambayo wahudumu wake hawana sifa  za kuendesha huduma hiyo na wengine wanatoa huduma za kuwachoma sindano wateja tofauti na kibali chao.

Ofisi ya Mganga Mkuu Ilala Daktar Sangu  imeweka utaratibu wake kila mwaka kufanya ziara ya ukaguzi  wa  kuzikagua maabara bubu ambazo hazina vibali na Maduka ya dawa mara baaada  ya kuwakamata imewataka wafuate taratibu za usajili ili kutoa huduma bora kwa wananchi wa Wilaya ya Ilala.

Sangu amesema katika oparesheni hiyo pia walifunga maduka ya dawa ambayo yalikuwa watoa huduma wasio na sifa na maduka mengine yakijiusisha na upimaji VVu,utoaji mimba na uchomaji sindano.

Hata hivyo amewataka watoa   huduma wote ambao wamekamatwa  kwenda Manispaa ya Ilala kwa ajili ya  taratibu  na usajili ili kuweza kufuata utaratibu.

Aidha amewataka wananchi watumie vituo vya tiba vilivyorasmi  Kwa ajili ya matibabu na maabara kwa ajili ya vipimo na maduka ya dawa kwa ajili ya kununua dawa  kwani hatua hiyo itaweza kuwapa   uhakika na  huduma wanazopewa  kwalengo la kulinda afya zao.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Manispaa  ya Ilala Dkt.Hawa Emily amewataka wamiliki wa vituo vya kutolea huduma katika wilaya hiyo, wafuate miongozo yote ya utoaji huduma ya Afya ili kuepusha  migogoro  kati yao na serikali.

Dkt .Hawa  amewataka  wamiliki watoe huduma kulingana na vibali vyao wasikiuke  kanuni,kikubwa wafuate miongozo  ya kukinga na kuthibiti maambukizi wakati wa utoaji huduma za afya.

Katika ziara hiyo ilifungia Maabara Bubu na Zahanati Kiwalani  Tabata, Kivule ,Minazi mirefu na kuwataka wamikiki wote kufuata taratibu za usajili.

Amina Omar