Serikali imetakiwa kujipanga vyema katika utoaji wa elimu bure

Skuli  za Serikali  Wilaya ya Mkuranga zinakabiliwa na Changamoto ya Miundo mbinu  ikiwemo  ukosefu wa  nyumba za Waalimu,Vifaa vya kufundishia,barabara, na  kupelekea Wanafunzi wa Skuli  hizo kufanya Vibaya katika Mitihani yao ya kuhitimu ikilinganishwa na shule  binafsi.

Akizungumza na Waandishi wa Habari Mkuu wa Wilaya Mkuranga Felberto Sanga  amesema  changamoto hizo  zinatokana na bajeti iliyotwengwa na serikali haijitoshelezi kukidhi   Mahitaji yote ya  Skuli  licha ya kutolewa elimu bure lakini bado  hali  ni mbaya kwa upande wa shule za serikali   na hali hiyo itapelekea  elimu kuendelea kudidimia kwa Upande  wa wanafunzi wanaosoma  skuli  za serikali.

Amesema Mazingira ya skuli hizo  siyo mazuri Walimu pamoja na Wanafunzi wanatembea umbali mrefu kufuata skuli  na kipindi cha mvua  wengine hawawezi  kwenda  Maskuli   kutokana na barabara kuwa mbovu.

Aidha amesema kwa Upande wa Afya nako hali ni Mbaya hakuna vifaa tiba,Upatikanaji wa Dawa Watumishi  ni  wachache hivyo serikali iangalie kwa makini  namna ya kusaidia Wilaya hiyo.

Amina Omar