Watanzania washauriwa kufuatilia historia ya nchi yao

Vijana nchini wameshauriwa kujijengea utamaduni  wa kufuatilia historia  ya nchi yao kujua kiundani asili yao kwa lengo la kufahamu  walipotoka na wanapokwenda ili kufanikisha kutunza amani ya nchi.

Akitoa ushauri huo  Mkurugenzi wa Kavazi la Mwalimu Nyerere Prof. Issa  Shavji   wakati wa  maonesho ya siku tatu ya Picha Adhimu na mijadala Juu ya Historia ya Ujenzi wa Taifa na Maendeleo yake.

Prof. Issa  Shivji amesema kuwa Lengo la Kavazi ya Mwalimu nyerere ni kuhifadhi Fikra za Mwalimu nyerere ziwe hai na kurithishwa kizazi hadi kizazi  kuvumbua historia na chimbuko la Taifa letu.

Kwa upande wake Mhifadhi Mkuu wa Nyumba ya Makumbusho ya mwalimu Nyerere Neema Mbwan  amesema kuwa maonesha hayo yanasaidi kuongeza elimu zaidi juu ya ufahamu wa historia ya taifa na namna ilivyo pata uhuru kutoka kwa mkoloni..

Ameongeza kuwa wanatarajia kufanya Maonesho hayo  katika mikoa tofauti nchini ili kuongeza uelewa zaidi kwa wananchi kufahamu historia ya Mwalimu nyerere pamoja na juhudi zake kwa Watanzania.

Amina Omar