Kundemba yajinasibu kubeba kombe Wilaya ya Mjini Unguja

Kocha  Mkuu wa timu ya soka ya Kundemba ya ligi daraja la pili  , iliyotinga hatua ya nne bora Wilaya Mjini Juma Yussuf Sumbu, amesema wamejipanga  vyema ilikuona wanauchukua Ubingwa  wa Wilaya hiyo.

Akizungumza na Zanzibar 24  kocha huyo, katika viwanja vya mazoezi Mnazi mmoja, alisema mazoezi ambayo wanaendelea kufanya anaamini wanaoweza kuondoka na Ubingwa huo ,bila ya wasiswasi wowote.

Alisema kuwa ,matarajio yao ni kufanya vizuri na kuondoka na Ubingwa ,huo ilikuipandisha timu hiyo daraja la pili Taifa  ndani ya Msimu wa mwaka 2018/2019

hata hivyo alisema Matarajio yao  kucheza mechi mbili hadi tatu za kirafiki na timu za vijiji , ilikuangalia viwango vya  wachezaji wa vijiji,

Kundemba ni miongoni mwa timu ya kwanza kati  ya timu nne ambazo zimetinga hatua ya nne bora katika Wilaya ya Mjini ambapo kwa sasa ligi hiyo imesimama baada ya vugu vugu la ZFA.