Kamal Manji, mdhamini mpya Gulioni FC

Mdhamini mkuu    Mpya wa timu ya Gulioni fc ya ligi daraja la pili Wilaya ya Mjini, ambayo imetinga hatua ya nne bora , Kamaly Manji kutoka Zanzibar ,amewaka mkataba wa makubaliano ya kuidhamini timu hiyo kwa muda wa misimu miwili ya ligi.

Akizungumza na Zanzibar 24 katika kikao cha kujadiliana juu ya udhamini huo ,huko ofisini kwake Mlandege alisema , udhamini huo utakuwa unahakikisha vitu vyote vinapatika katika timu hiyo.

Hata hivyo, katika udhamini huo  aliwahidi viongozi wa timu hiyo,  kufanya kila hali ilikuhakkisha  timu hiyo inapanda daraja  la Pili Taifa ndani ya msimu wa -2018/2019

Mdhamini huyo aliwahidi viongozi hao kuwapatia vifaa vyote  vya wachezaji kuanzia viatu, jezi ,soksi, shin gadi na vitu vyengine ,ambavyo vitawasaidia  kufanya vizuri katika mashindano yao.

Alisema vitu hivyo ambavyo ameiahidi atavikabidhi  kwa  wahusika ndani ya siku tano ,ilikuona anatimiza  ahadi ambazo aliweka kwa  viongozi hao.

Aidha Kamaly Manji aliwataka viongozi, wachezaji pamoja na mashabiki wa timu hiyo, kutarajia mazuri kutoka kwake katika misimu hiyo.

Alisema kuwa lengo la kuidhamini timu hiyo ni kuisadia kutokana na utendaji mzuri wa soka ambalo wamelionesha ndani ya timu yao.

Mbaraka Himid aliekuwa Rais wa timu ya Mlandege ,amesema tayari amesha rudi katika timu yake ya dhamani, hivyo ameahidi kutoka mashirikiano ya pamoja ,ilikuona wanaipandisha daraja timu hiyo.

Akizungumza kwa niaba ya  uongozi wa timu  hiyo Rais wa timu hiyo ,Ahmed Khamis Ali,amemuahidi  mdhamini huyo, kufanya kazi  kwa pamoja ,ilikuona timu inakuwa mzuri kulikozi timu zote za Zanzibar.

Hata hivyo alisema kuwa ujio huo uliwafurahisha ,mashabiki,viongazi na wachezaji wa timu hiyo, hivyo wamemtaka mdhamini huyo kutambua kuwa timu hiyo ,ipotayari kuwafanya mazuri katika mashindano yao yote

Gulioni fc ni miongoni mwa timu ambayo imetinga hatua ya nne bora kwa Wilaya ya Mjini Unguja msimu huu kutafuta Bingwa wa Wilaya hiyo.