Mashindano ya ZAHLIFE kuanza kutimua vumbi mwisho wa mwezi huu

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dk Ali Mohammed Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi kwenye ufunguzi wa mashindano ya Taasisi ya Elimu ya Juu na Vyuo Vikuu Zanzibar (ZAHLIFE) yanayotarajiwa kuzinduliwa rasmi Ijumaa ya tarehe 29 juni 2018.

Akizugumza na Zanzibar24 Katibu Mkuu wa kamati ya Habari na Michezo ya ZAHLIFE Masud Juma Abdul Rahman amesema maandalizi kwa upande wa mashindano tayari yameshakamilika na vyuo vyote tayari vimeshawasilisha majina ya wanafunzi watakaoshiriki mashindano hayo.

Aidha Masudi ameelezea mashindano ya ZAHILIFE Cup yapo kwa ajili ya kujenga uhusiano baina ya vyuo na taasisi hiyo ili kuondoa changamoto zinazoikumba elimu ya juu Zanzibar.

“Tumejipanga kuhakikisha kundoa lawama za mamluki kila siku zinalalamikiwa na vyuo vingi kwenye mashindano haya” Alifahamisha Masudi.

Kwa upande mwengine Masud ameeleza jumla ya vyuo kumi na tatu vinatarajiwa kushiriki katika mashindano hayo kwa jinsia zote wanawake na wanaume na vyuo vitatu vimejitoa katika mashindano hayo.

“ Vyuo kama vile Melisha training, Zibret, na Kizimbani wamejitoa kwenye mashindano haya kwa sababu mbalimbali ikiwemo ya mitihani” Alifahamisha Masud Juma ambaye ni Katibu wa kamati ya Habari na Michezo.

Mashindano ya ZAHLIFE CUP yanatarajia kunza wiki ijayo ya Tarehe 29 na kuhusisha michezo mbali mbali ikiwemo ya mpira wa miguu, mpira wa mikono ,Riadha,na mengine mengi.

Aidha kwa upande wa udhamini Masudi ameeleza kuwa tayari wamesha peleka maombi kwa taasisi mbali mbali ikiwemo ZSSF, NMB Bank na nyenginezo na alidai muelekeo unaelekea kuwa mzuri.

Mwaka jana mashindano hayo yalifunguliwa na Makamo wa Pili wa Raisi Balozi Seif Ali Iddi na Chuo cha Zanzibar University (ZU) waliibuka kuwa mabingwa wa mashindano hayo baada ya kuifunga chuo cha Afya , kwa upande wa wanawake Mwenge waliibuka mabingwa wa mchezo wa Nage kwa kuiondosha Chuo Cha Habari Zanzibar (ZJMMC).