ZRB kuanzisha mfumo mpya wa ukusanyaji kodi Mahotelini

Bodi ya Mapato Zanzibar (ZRB) imesema kuanzishwa kwa mfumo wa mashine ya Elektronik katika sehemu za hoteli itasaidia Kuimarisha ukusanyaji wa mapato na kuondosha usumbufu kati yao na walipa kodi.

Akizungumza katika mafunzo ya wafanyakazi wa hoteli Meneja wa sera, Utafiti na Maendeleo ya Bodi  ya Mapato Zanzibar,(ZRB) Ahmed Sadat Haji alisema uanzishwaji mfumo huo utaweza kuisaidia bodi hiyo kupata taarifa za usahihi kwa wageni watakaoingia katika hoteli hizo.

Alisema lengo la kuanzishwa mfumo huo, utaweza kurahisisha utendaji wa kazi zao katika pande mbili na kuepusha matatizo wakati wa kulipa kodi ya serikali.

Aidha alisema Bodi hiyo imekuwa ikifanya ziara za kuzitembelea hoteli mbalimbali kwa lengo la kutoa elimu ili kuweza kuzitumia mashine hizo ipasavyo.

Mbali na hayo aliwataka wafanyakazi hao kutumia  matumizi ya mfumo mpya wa mashine ya Elektoniki  (FCR),ambayo itawarahisishia kazi zao katika ulipaji wa kodi na kutunza kumbukumbu.

Alisema lengo la mafunzo hayo ni kuitambulisha mfumo huo, ambao utakuwa unatumika katika Hoteli zote za Zanzibar, ilikuondosha matatizo ambayo hujitokeza kwa wafanyakazi na walipa kodi wa Bodi hiyo.

Hata hivyo,  alisema lengo jengine ni kutoa mafunzo mafupi  kwa wafanyakazi hao, ilikufahamu matumizi ya  mashine hiyo ,ambayo itawarahisisha katika kazi zao na kujua kumbukumbu za kazi zao.

Aidha alisema mbali na hayo watakuwa na ziara ya kitaaluma kwa walipakodi wa Hoteli  hizo ,ilikuendelea kutoa mafunzo na kuhakikisha kila mfanya kazi anafahamu matumizi ya mashine hiyo.

Maneja wa Mradi wa mashine  za Hoteli  za kukusanya mapato na kutunza kumbukumbu  kutoka ZRB, Mussa Amour, alisema mashine hizo zitasaidi kuondosha matatizo yote ambayo yalikuwa yakijitokeza mara kwa mara kwa walipa kodi  na wafanyakazi wao wa Bodi hiyo.

Alisema kuwa muda mrefu uwekaji wa kumbukumbu ulikuwa mbovu, na ulikuwa unasababisha usumbufu kwa wateja wao , ambapo kuwepo kwa mashine hizo utaweza kusaidia.

Nae mkufunzi wa mafunzo hayo, Shabani Yayha aliwataka wafanyakazi hao kutuzitumia mashine hizo kwa uwangalifu zaidi,ili kuona wanaondokana na changamoto zilizokuwa zikiwssumbua kwa muda mrefu.

Nao washiriki wa mafunzo hayo, waliipongeza bodi hiyo kwa kuwapatia mafunzo ambayo yataweza kuwasaidia katika kuhifadhi kumbukumbu za kazi zao.

Mashine hizo zinatarajiwa kutumika Jalai mosi mwaka huu.