Video: Barnaba afunguka kumpa pesa mwanamke si kumhonga

“Mwanaume kumpatia mwanamke fedha si kuhonga bali ni zawadi kitu ambacho ni kawaida katika maisha yake ya kila siku”.

Msanii wa Bongo Flava, Barnaba anayefanya vizuri na wimbo wake mpya ‘Chausiku’, ametoa kauli hiyo wakati akipiga stori na Wasafi TV na kusema mwanaume kumpatia mwanamke fedha ni sawa na kumwagilia maua.

“Nahonga sana kaka na mpaka sasa nahonga, nawachukia wanaume wenzangu wanaosema kuhonga. Mwanamke ukimpa kitu, pesa au talanta yoyote yenye thamani haiitwi kuonga, mwanamke unamzawadia,” amesema.

“Mwanamke ni pambo ambalo linatakiwa kumwagiliwa, ukimpa mpenzi wako pesa umemwagilia ua lako, ume-protect tunda lako, mwanamke anahitaji kutunzwa, usimpomtunza mwenzako watakutunzia,” amesisitiza Barnba.

Video: Barnaba afunguka kumpa pesa mwanamke si kumhonga.

 

Barnaba yupo mbioni kuachia albamu yake mpya ‘Gold’ ambayo itakuwa na nyimbo zipatazo 18. Wasanii walioshiriki katika albamu hiyo ni pamoja na Juliana Kanyomozi na Jose Chameleon kutoka Uganda. Kutoka Bongo kuna Vanessa Mdee, G Nako, Ben Pol, Aslay, Barakah The Prince, Linex na Joh Makini.