Makamo wa Rais: Rushwa inaumiza maskini

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amesema “Tanzania chini ya Serikali ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli inajitahidi sana kupambana na rushwa pamoja na viashiria vyake”

Makamu wa Rais ameyasema haya wakati wa kujadili Kaulimbiu ya  Umoja wa Afrika kwa mwaka 2018 “Kushinda Vita dhidi ya Rushwa: Njia endelevu ya mabadiliko ya Afrika” katika Mkutano wa kawaida wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika unaomalizika leo mjini Nouakchott, Mauritania.

Makamu wa Rais amesema rushwa inaumiza watu hususani watu masikini na kudhoofisha ukuawaji wa uchumi hivyo ni vyema rushwa ipingwe kwa nguvu zote.

Aidha, Makamu wa Rais amesema Tanzania inatambua vita dhidi ya Rushwa inahitaji jitihada za pamoja katika ngazi zote ikiwemo Kitaifa, Kikanda na Bara zima.

Katika mkutano huo ambao umejadili mambo mbali mbali, Tanzania itaendelea kushiriki katika kutatua migogoro kwa njia ya mazungumzo

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akichangia maoni ya Tanzania juu ya masuala ya Ulinzi na Amani katika nchi za Burundi, Congo DRC, na Sudan ya Kusini wakati wa mkutano wa kawaida wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika (AU)mjini Nouakchott, Mauritania. (picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Jaji wa Mahakama ya Afrika ya Binadamu na Watu Jaji Imani Mkwawa Aboud wakati wa mkutano wa 31 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika mjini Nouakchott, Mauritania. (picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)