Kikosi cha Kombaini kitakachochuana mashindano ya Rolling Stone Mkoani Arusha

Kocha mkuu wa Timu ya Kombaini ya wilaya ya mjini Muhamed Seif King ametangaza majina ya wachezaji ishirini watakaounda kikosi hicho kinacho tarajia kuelekea  kwenye mashindano ya Rolling Stone Mkoani Arusha Mwezi huu.

Akikitangaza kikosi hicho kinacho husisha wachezaji wenye umri wa miaka 13 hadi 17 kwa mujibu wa kanuni ya mashindano hayo.

Kocha Seif King amewatangaza Walinda Mlango Mwinyi Ali, Ahmada Abdulrahman NA Kwa upande wa Walinzi Abdallah Saidi, Abdulahamid Ramadhan, Mudathir Nassor, Mussa Mohamed, Mohamed Haji, Khalid Khamis,Makame Mohamed na Abubakar Suleiman.

Kwa upande wa Viungo wameitwa Yahaya Silima, Fahad Mussa, Kassim Suleiman, Mustapha Muhsin, Yassir Ali, Ibrahim Ali , na Mohamed Khamis NA washambuliaji ni Ibrahim  Yahya , Nassor Saleh, Yussufu
Bwanga, Muhamed Daudi na Yussufu Saidi Jussa

Aidha Kocha Seif King amesema kikosi hicho kinaendelea na mazoezi uwanja wa Amani na kinaendelea kujipima mechi za kirafiki na vilabu mbali mbali .

Kombaini ya wilaya mjini itakwenda kwenye mashindano hayo kama Bingwa mtetezi baada ya kufanikiwa kuchukua ubingwa wa mashindano hayo ya Rolling Stone mara mbili mfulilizo mwaka 2016 na 2017.