Matokeo ya michuano ya soko vyuo vikuu Zanzibar

Mashindano yanayo simamiwa na taasisi ya elimu ya juu vyuo vikuu imeendelea leo katika raundi yake ya pili katika viwanja mbali mbali, ambapo katika uwanja wa chuo cha afya (MBWENI) uliwakutanisha chuo cha uwandishi wa habari (ZJMMC)na chuo cha utumishi wa umma( IPA) ambapo ZJMMC imepigwa
kipigo cha mabao kumi bila majibu.

Magoli ya IPA yamefungwa na Mohd Othman dakika ya 14, Wahid Abdi 16, 37,Talib Hamad Makame dakika ya 35,68, Abdulizzat Ayoub  dakika ya 50, 54,Kitwana Hassan dakika ya 60,Hassan Alli dakika ya 75, na Abrahman dakika ya 90 .

Chuo cha Sumait kimepokea kichapo cha mabao matatu kwa moja dhidi ya chuo cha kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere katika uwanja wa chuo cha Zanzibar University (ZU),SUZA wamepata alama za mezani baada ya chuo kikuu huria kuingia mitini .

Mzunguko wa tatu wa mashindano hayo unatarajiwa kuendelea kwa kuchezwa michezo mbali mbali Icps vs Sumait katika uwanja wa Karume, Mwalim Nyerere na SUZA katika uwanja wa Zanzibar University(Tunguu),

Zanzibar School Health dhidi ya Chuo cha Ufundi Karume uwanja wa chuo cha Afya Mbweni, Microtech dhidi ya Chuo cha Uandishi wa Habari uwanja wa chuo cha Sumait.