Wanamichezo wa kuinua vitu vizito Zanzibar walia na Serikali

Chama cha kuinua vitu vizito Zanzibar (The Zanzibar Weight Lifting Association) body building kimeiomba Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar na wadhamini kuwasidia ili kuendelea kuwakilisha Zanzibar kwenye mashindano ya kimataifa kwa mafanikio zaidi .

Akizugumza na Zanzibar24 Raisi wa Chama hicho Bakar Hashim Bakar amesema wao ndio chama pekee kinachowakilisha Zanzibar kwenye mashindano ya kimataifa na kuleta mafanikio makubwa kwa upande wa Zanzibar kwani mchezo huo vifaa vyake vinagharimu fedha nyingi sana.

Mwandishi wa zanzibar 24 iibrahim Makame akiwa na Raisi wa chama cha kubeba vitu vizito zanzibar

Aidha kwa upande mwengine Bakar Hashim ameeleza kwa upande wa vilabu Zanzibar vipo vingi lakini havijawa na uelewa wa kujisajili licha ya jitihada wanazozifanya lakini vilabu vinne tu ndio vilivyojisajili kwa mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar.

Ameendelea kufunguka kwa kusema wameshiriki mashindano mingi ya kimataifa na kuchaguliwa kuwa  mwanachama kamili wa mchezo huo baada ya kumalizika mashindano ya Dunia kule Cameroon na kuonekana Zanzibar na kukabidhiwa uanachama kamili wa World Body building and Physique
Fedaration (WBPF).

“Ukweli kuna vilabu vingi Zanzibar lakini kuna watu wanaingilia kati bila ya kujua taratibu watu wenye vilabu binafsi huwalipisha ada nyingi wachezaji kuona ni biashara huu ni mchezo kama mchezo mwengine” Alifahamisha Bakar Hashim.

Amefahamisha kuwa hakuna mtu mwenye mamlaka ya kuingilia mchezo huo wa kutunisha misuli badala yao chama cha mchezo huo ili kuondoa hatari za mchezo huo zinaweza kuwakumba wachezaji wa mchezo huo.

“Tumeshiriki kwenye michezo mingi ya kimataifa kule Cameroon, Dubai, Uganda na ndani ya nchi“ Alisema Bakar Hashim.

Aidha amesema wamejipanga kufanya mashindano makubwa ya ndani ili kushawishi jamii na kuwavutia wadhamini kwa kuwa mchezo huo unakumbwa na changamoto nyingi ikiwemo kusafirisha wachezaji kwenye mashindano hayo ya kimataifa ni gharama .

Kwa upande wake mchezaji wa mchezo wa kuinua vitu vizito Joma Jaku amesema mchezo huo unachangamoto ya vifaa ambavyo ni gharama hawawezi  kuvigharamia kama wao wachezaji huchangishana na kununua vifaa hivyo .

“Nimeshiriki michezo mingi ya kimataifa ya Afrika kule Misri,Uganda na ile ya Afrika Mashariki tunajifunza mengi wenzetu wamejipanga kiushindani kwa kuwa na vifaa imara na vya kisasa”  alimalizia Joma Jaku.