Huu hapa Ujumbe wa Birthday wa DiamondPlatinumz kwa Mama yake: Amuahidi nusu ya mali zake

DiamondPlatinumz kwenye vichwa vya habari tena ikiwa ni siku ya kuzaliwa ya Mama yake maarufu Mama Dangote. Haya hapa ndiyo aliyoyaandika kupitia ukurasa wake wa instagram

Nasikitikaga sana Wanapojaribu Kulinganisha Thamani yako kwangu na Mtu yoyote…Na kusahau kuwa pasipo wewe kunizaa na Kunilea kwa shida na tabu leo hii hakuna yoyote ambae angeniona wamaana….. Ikiwa wewe ndio Ulonifanya mie nikawa Duniani Basi you will always be My First priority then the rest will follow…Dharau na Manyanyaso Ulopitia kwenye kunilea Hakuna anayejua, Tabu na shida Ulizopitia kufanya hadi leo walau nionekane mtu mbele za watu.. eti mtu kirahisi tu anatokea na kukuringanisha na mtu… Mama MADALE is your House!!! na ikitokea kesho nimekufa pia NUSU ya Mali zangu zote ni zako.“ameandika Diamond Platnumz.

Mwanao Napambana Usiku na Mchana Kwanza kwajili yako, Walau Ujifariji kwa Magumu Ulopitia kwa kunilea kwangu, i want you to Enjoy the life as Much as You can, Maana sina cha kukulipa zaidi ya Hicho..HAPPY BIRTHDAY MAMA I LOVE YOU SANA,“.