Young Basketball Association yasimamishwa kufanya Shughuli za michezo

Chama cha mpira wa kikapu Zanzibar (BAZA) kimeisimamisha shughuli za michezo zinazofanywa na taasisi ya Young Basketball Association (ZYBA) kwa sababu ya kutokuwa na mamlaka ya uendashaji wa michezo wa mpira wa kikapu Zanzibar kwa mujibu wa sheria.

Barua iliyosainiwa na katibu mkuu chama cha mpira wa kikapu Zanzibar AbdulRahman Mohamed Hassan alisema tasisi hiyo imesamamishwa kwa kutofautiana na Baraza la michezo la taifa la Zanzibar (BMTZ) na kanuni ya mpira wa kikapu Zanzibar, chama cha mpira wa kikapu Zanzibar ndio wenye maamlaka ya kuendesha shuguhuli za mpira wa kikapu Zanzibar.

Kwa upande wake makamo mwenyekiti wa chama cha mpira wa kikapu Zanzibar Rashid Hamza Khamisi amesema chama kimechukua hatua hiyo ili kulinda heshima kwa kuepusha migogoro inayoweza kutokea.

Aidha amesema Katiba ya chama hicho inasema wazi kuwa chama hicho ndio chenye mamlaka ya kuendesha shughuli za mpira wa kikapu pekee kwa upande wa Zanzibar na kuwataka wadau wa mchezo huo kufuta utaratibu na
kutokwenda kinyume na kanuni za chama hicho.

Aidha mwisho aliwaomba wadau wanao taka kuendesha shughuli za mpira wa kikapu Zanzibar kuonana na uongozi wa BAZA ili kuondoa migogoro na atakae enda kinyume na utaratibu hatua za kisheria zitachakuliwa.