Chuo cha Mwalimu Nyerere chaibuka kidedea ushairi ZAHLIFE

Bonanza la mashindano yanayosimamiwa na taasisi ya Vyuo vikuu Zanzibar na Elimu ya juu (Zahlife) likiwa linaelekea mwishoni kwa michezo mbali mbali Chuo cha kumbu kumbu ya Mwalimu nyerere kimeibuka ushindi wa mwanzo  wa mashindano ya Ushairi wa lugha ya Kiswahili kwa kupata alama 82.0  dhidi ya vyuo vya State University of Zanzibar (SUZA), Chuo cha Ualimu Sumait na Chuo kikuu Huria kanda ya Zanzibar.

Jumla ya washiriki wanne wameshiriki kwenye mashindano hayo yaliofanyika kwenye holi la ukumbi wa Chuo Cha Uandishi wa Habari Zanzibar Kilimani  yaliyosimamiwa na kamati ya sanaa na mashairi ya Zahlife .

Matokeo ya jumla ya mashindano hayo SUZA wamepata alama 65.67 na kuchukua nafasi ya tatu, Chuo Kikuu Huria wamepata alama 68.67 na kuchukua nafasi ya pili, Sumait wamepata alama 64.67 wamachukua nafasi ya nne na Chuo cha kumbu kumbu  ya Mwalim Nyerere wamechukua nafasi ya kwanza kwa kupata alama 82.0 .

Kwa upande wake Katibu mkuu wa kamati ya Habari na Elimu na Michezo wa Zahlife Masud Juma amesema licha ya mashindano hayo kuonekana ni madogo kwa baadhi ya vyuo vimekuwa vinashindwa kuwandaa wanafunzi wao
kitaaluma ya Ushairi wa Kiswahili na kushindwa kushiriki katika kinpengele hichi muhimu.

“ Ushairi wa kiswahili leo umevutia kwa aina ya mada zilizowasilishwa kama vile madawa ya kulevya ulio wasilishwa na SUZA na hata ule wa Mwalim Nyerere wa udhalilishaji unaweza kujenga jamii mpya kwa Zanzibar hususan kwa ngazi yetu ya taaluma” Alimaliza Masudi Juma.

Mashindano ya Zahilfe yanatarajia kumaliza wiki ijayo kwa ngazi ya Fainali na kufuatiwa na mashindano mbali mbali kama vile Riadha, mbio za magunia, mashindano ya kunywa soda na mashindano mengine. Mashindano hayo ya mwaka huu 2018 yamebeba ujumbe wa “Vijana Shiriki michezo kupiga vita rushwa na ubadhilifu wa mali ndani ya tasisi za serikali”.