Mhe. Samia aongoza kikao cha kamati maalum ya halmashauri kuu CCM Zanzibar

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo Julai 09, 2018 ameongoza kikao Cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar katika ukumbi wa mikutano Afisi Kuu CCM Zanzibar.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kwenye ukumbi wa Afisi Kuu Zanzibar, kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe.Balozi Seif Idd na kulia ni Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Sadalla.

Kikao hicho kilichobeba ajenda kuu mbili, ambazo ni Mapendekezo ya Kupiga Kura za maoni katika uchaguzi wa Jimbo la Jang’ombe na Mapendekezo ya Wanachama wa CCM wanao omba kuteuliwa kugombea nafasi ya Uwakilishi jimbo la Jang’ombe.

Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akisoma Ilani ya Uchaguzi ya CCM wakati kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar kwenye ukumbi wa Afisi Kuu CCM Zanzibar, kushoto ni Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar Mhe.Balozi Seif Idd 

Mwenyekiti wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Dkt. Ali Mohammed Shein yupo safarini nje ya nchi hivyo wajumbe walimchagua Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kuwa Mwenyekiti wa muda na kuongoza kikao hicho.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dkt. Abdalla Juma Sadalla akisoma ajenda zitakazojadiliwa kwenye Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar.

 

Wajumbe waliohudhuria Kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Zanzibar.
Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais.​