Masharti ya NEC kwa wapiga kura uchaguzi mdogo

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imevitaka Vyama vya siasa na Wagombea wote wanaotarajia kushiriki katika Uchaguzi Mdogo utakaofanyika 12,agosti,2018 kufuata taratibu na sheria na Madili  ya Uchaguzi na Chama chochote.

Mgombea yeyote,Afisa yoyote wa Uchaguzi au mwananchi yeyote atakayekiuka adhabu na hatua mbalimbali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.

Akizungumza na waandishi wa habari Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi MHE. JAJI SEMISTOCLES KAIJAGE amesema fomu za Uteuzi zitatolewa kuanzia julai 8 hadi 14,2018.
Uteuzi wa Wagombea utafanyika tarehe 14 julai, 2018 ambapo Kampeni za Uchaguzi zitaanza 15 julay,2018 na kumalizika 21Agost,2018 na Siku ya Uchaguzi itakuwa 12 Agost,2018.
Amesema Uchaguzi huo Mdogo wa Ubunge na Udiwani unahusisha Jimbo LA Buyungu Halmashauri ya Kakonko na Udiwani kwenye kata 79 zilizopo katika Halmashauri 43 kwenye mikoa 24 ya Tanzania Bara
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Tume ya Uchaguzi DK ATHUMANI KIHAMIA amesema Jukumu la kutangaza Matokeo ni la Tume na sio kila Mtu anaweza kutangaza Matokeo Utaratibu wa Uchaguzi
Aidha amesema Mpiga kura aliyepoteza kadi yake ya kupiga kura au ambaye kadi yake imeharibika au kuchakaa aweze kuruhusiwa kutumia vitambulisho vilivyoruhusiwa na Tume kama lesseni ya gari Kitambulisho cha Utaifa na Kadi ya kusafiria(viza).