Timu ya JKU kufika nusu fainali Kagame CUP ni matumaini kwa Wazanzibari

Mabingwa watetezi wa ligi kuu ya Zanzibar JKU wamefuzu kwa mara ya kwanza nusu fainali ya michuano ya Kagame Cup baada ya kuitoa Singida United kwa mikwaju ya Pelnat mitatu kwa Minne.

Hongera za pekee kwa Mlinda mlango wa JKU  Abrahman Mohamed (Wawesha) kwa kufanikiwa kuokoa michomo mengi katika mchezo huo ambao Singida United chini ya mkufunzi Hemed Suleiman Moroko walielemea lango la Jku kwa kipindi cha kwanza.

Wengi waliona Jku wanakwenda kuwakilisha Zanzibar sio kushindana Kwa kuona maandalizi ya timu hiyo hayakuwa makubwa kama vile yanvyo tarajiwa ila kwa hatua waliofikia Jku wanahitaji kupongezwa kwa kuwa miongoni mwa Timu ambazo hazijapewa nafasi ya kufanya vizuri kwenye michuano hiyo mikubwa Afrika Mashariki na Kati.

Dawati la michezo Zanzibar24 tunakupeni hongera za kutosha, tunakuoneni nyinyi ni mashujaa ambao hamuwezi kushindwa vita kama jina la timu yenu linavyo beba uzito wa kazi yenu katika jamii.

Mafanikio yenu mpaka hapo mlipo ni msingi mzuri wa mandalizi ya klabu kwa kuona kuna haja ya kuwa na Acedemy ya mpira wa miguu ndani ya kambi ya skuli yenu ya Jku  ni jambo zuri na kubwa ambalo kwa muda mrefu Zanzibar tumelikosa.

Hatua mliyofikia ni wazi Jku mlikuwa mnasifa ya kuitwa mabingwa wa ligi kuu ya Zanzibar na kutoa wachezaji wengi kwenye timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heros) kwa kuwa ndio timu inayobeba nyota  wengi wa mpira wa Zanzibar kama vile Feisal Salum, Issa Haidar, Abrahman Mohamed, Amur Suleiman, Edward Peter Mayunga na wengine wengi hivyo mnahitaji pongezi  kwa juhudi zenu binafsi.

Lakini bado mnasafari ndefu dhidi ya mchezo wa Simba katika hatua ya Nusu Fainali mnahitaji kuongeza kasi ya mashambulizi zaidi na kuhakikisha mnapata matokeo uwanjani ili kuongeza hamasa kwa wale
ambao kabla ya safari yenu labda walikuwa wakiwabenza kwa kuona mnakwenda kuwakilisha tu.

Hongereni klabu ya Jku wakilishi wetu kutoka Zanzibar dawati la michezo Zanzibar 24 tunakupeni Hongera na kukutakieni kila la kheri kwenye hatua ya nusu Fainali dhidi ya Simba nyie ndie mtakao beba
matumaini ya wazanzibar walio wengi tunathimi juhudi zenu  ili kuleta mafanikio kwa wazanzibar.