Watengezaji filamu Kenya waitaja Lugha ya kiswahili ni kikwazo

Lugha ya kiswahili ni moja ya changamoto zinazowakumba watengezaji wa filamu nchini Kenya.

Hayo yamebainishwa na watengenezaji wa filamu wa kampuni ya Bill Afwani ya Kenya Njue Kevin na Phoebe Ruguru wakati wakizugumza na wandishi wa Habari  katika Hoteli ya African House huko
Vuga mkoa wa Mjini magharibi Unguja katika Shamra shamra za Tamasha la Filamu Zanzibar (ZIFF).

Wamesema kwa muda mrefu watengezaji wa filamu wa Kenya wamekuwa wakijaribu kutumia lugha ya Kiswahili lakini filamu zao zimekuwa zinashindwa kufanya vizuri.

Aidha kwa upande wa changamoto za utengenezaji filamu Kenya Njue Kevin amesema wamekuwa wakikumbwa na changamoto ya lugha ambayo waigazaji wengi wapya wamekuwa wakishindwa kutumia lugha ya Kiswahili ambayo usiklizwaji wake ni mdogo.

Phoebe Ruguru kwa upande wake amesema filamu za Tanzania zinaweza zikawa bora kama zitatengenezewa maeneo mazuri na wazalishaji kuongeza ubora wa kazi zao ili kushindana kimataifa kwenye ulimwengu wa filamu.

Aidha wamewataka wadau wa filamu Afrika Mashariki kuhakikisha wanatengeneza soko la pamoja la filamu ili kuhakikisha filamu za Afrika Mashariki zinakuwa bora na kuwa na mazingira ya kweli yanayo
endana na uhalisia wake.

Kwa upande wake Mkuregenzi muendashaji Claus plus Ramadhan Bukini amesema wao kama wadau filamu Tanzania wataendelea kuzitangaza filamu za Tanzania ikiwa wataendelea kupata mashirikiano na wadau wa Filamu Afrika Mashariki ikiwemo watengenezaji.

Tamasha la filamu la kimataifa la 21 Zanzibar(Zanzibar International Festival) linaendelea visiwani Zanzibar baada ya kufunguliwa rasmi na Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi Issa Haji Gavu na jumla ya wageni
mia sita wanatarajiwa kuingia Zanzibar na maenesho ya filamu mbalimbali zikiendelea maeneo tofauti na kilele chake  tarahe 15 mwezi huu.