Waziri wa habari awapa tumaini Wasanii wa muziki wa Asili Zanzibar

Wasanii wamuziki wa Asili kutoka  visiwani    Zanzibar wametakiwa kuendeleza na kudumisha utamaduni wao   kupitia  Muziki    huo ili kuona  wanaitangaza Zanzibar ndani na njee ya nchi katika sula la muziki waasili.

Kauli hiyo imetolewa na Waziri wa Habari Utalii na Mambo ya kale Mahmoud Thabit Kombo, wakati akizungumza na wasanii hao katika zoezi la ukabidhi wa vifaa vya muziki wa kale katika  chuo cha muziki cha DCMA kilichopo Forodhani  Mjini Unguja.

Alisema utamaduni wa muziki  waasili  ni miongoni  mwa mambo ambayo wanajivunia  katika  visiwa  vya Zanzibar kwa muda mrefu na kuwataka wasanii wa muziki wa asili kuchangamkia fursa  zinapojitokeza  ili kuendeleza   vipajivyao.

Hivyo amewataka  wasanii hao Kuendelea kutoa mashirikiano Kati yao na nchi ya Pakstani kwa lengo la  kuudumisha mziki huo Kwani utamaduni wao ndio utambulisho wa nchi yao.

Alisema lengo la Serikali kuona wasanii wa Zanzibar wanakabidhi mambo mawili hadi  matatu ambayo yatatumiwa katika kuendeleza kazi zao.

Nae balozi  kutoka  nchini Pakstani Hazem Mshabat aliwaahidi wasanii hao kuwarejeshea mahusiano yao mbayo yalipotea kwa muda mrefu kati yao na Wasaani wa Pakstani na kuwapatia vifaa vyengine vyakuendelza muziki wao .

Kwaupande wake Mkurugenzi wa chuo cha muziki wa asili (DCMA) Adrian Podgorny, aliwaahidi wasanii hao kuwa mashirikiano yao na wapakstani yataendelea Ijapokuwa  Balozi takuwepo Nchini Nairobi.