ZU yarudi na ushindi wa tatu michuano ya Vyuo vikuu vya Afrika

Wawakilishi wa Zanzibar kwenye michuano ya Vyuo vikuu vya Afrika, Zanzibar Univesertiy wamerejea visiwani hapa wakishika nafasi ya Tatu kwenye mashindano hayo ya Afrika kwa ngazi ya Vyuo kule Makelele Ethopia.

Akizugumza na Zanzibar24 baada ya timu hiyo kuwasili katika Bandari ya Zanzibar Kocha mkuu wa Timu hiyo Yussufu Juma (Kocha Sumbu) amesema anawapongeza vijana wake kwa bidii kubwa waliofanya hadi kufanikiwa kupata nafasi ya tatu kwa kuwa mashindano hayo yalichezwa kwa makundi na kutafuta alama si mtoano.

Aidha kwa upande mwengine Kocha Sumbu amesema hakukuwa na timu nyigi kwenye mashindano hayo lakini ushindani haukuwa mkubwa kwa kuwa ameshinda michezo yote 4 na kufungwa mchezo moja na sare mmoja lakini walikuwa na alama sawa na chuo cha Uganda ingawa tofauti ya magoli.

“Sisi Tumepata nafasi ya tatu tunawaomba wazanzibar na Serikali watambue sisi tumerudi na lakini bahati mbaya hatukakabidhiwa bendera ya nchi” Alisema Kocha Sumbu.

Kwa upande mwengine amesema mashindano hayo kila timu ilikuja na Bendera yake si kama chuo bali walikuja kama timu ya nchi lakini wao hawakuandaliwa mazingira mazuri ya safari licha ya kuangwa
lakini bado hawakupewa kipao mbele kama wawakilishi kutoka Zanzibar na Tanzania yake.

Kwa upande wake Kaimu mkuu wa idara ya Elimu Michezo division ya Elimu ya juu Abdalla Juma Abdalla amesema wao kama wizara wamejitokeza kuipokea timu hiyo na muelekeo wa mafanikio ya mashindano ya maskulini Zanzibar ya Elimu bila ya malipo na kwa ngazi ya Msingi na Elimu ya Juu Zanzibar.

“Hawa vijana tumewazalisha sisi wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali na leo ndio tunasherekea mipango yetu ya kuendeleza michezo ili kuendeleza vipaji vyetu” Alisema Abdalla.

Chuo cha Zanzibar University kinatarajia kwenda tena kwenye mashindano ya Vyuo vikuu vya Afrika mashariki na kati kama Bingwa mtetezi wa mashindano hayo mwezi wa Tisa mwaka huu huko mjini Dodoma.