ZAWA yakiri kuwepo kwa shida ya maji katika baadhi ya maeneo ya wilaya ya magahribi A na Kaskazini B

Wananchi wametakiwa kuwa wastahamilivu juu ya ukosefu Wa huduma ya  maji safi na salama katika baadhi ya maeneo ya wilaya ya magahribi A na Kaskazini B

Hayo yameelezwa na Afisa wa Uhusiano wa Mamlaka ya maji Zanzibar (ZAWA) Zahor Suleiman wakati Akizungumza na Zanzibar24  amesema kuwa ukosefu wa huduma hiyo inayosababishwa na ubovu wa tangi la maji pamoja na kupasuka kwa mabomba ya maji  hali ambayo inapelekea kuwepo kwa usumbufu katika huduma hiyo ya maji na salama

Aidha, Zahor amefahamisha kuwa kutokana na matatizo hayo wakaamua kuweka mgao wa maji katika maeneo hayo ili kuwaondolea usumbufu unaojitokeza kwa wananchi.

Hata hivyo Zahor amesema katika kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo uko mradi wa warasihema wa kuchimba visima pamoja na ukarabati wa nyundo mbinu ya maji ili kuliondoa tatizo hilo katika maeneo.

Rauhiya Mussa Shaaban