Shirika la Umeme Zanzibar ZECO latangaza nafasi za kazi

TANGAZO LA KAZI.

Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) linakaribisha maombi ya kujaza nafasi tupu katika kada mbali mbali kwa waombaji wenye sifa stahili kwa ajili yaUnguja na Tawi la Pemba kama ifuatavyo: –

UNGUJA

1. MHANDISI UMEME (ELECTRICAL ENGINEER) Nafasi – 2

Sifa za Muombaji

i. Awe amaehitimu na kupata Shahada au Stashahada ya juu katika fani ya Umeme (Degree or Advance Diploma in Electrical Engineering or Electrical and Electronics Engineering).
ii. Umri usiozidi miaka 40 ifikapo mwezi wa Agosti 2018.
iii. Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

2. FUNDI MCHUNDO (ELECTRICAL TECHNICIAN) Nafasi – 2
Sifa za Muombaji
i. Awe amehitimu na kupata Stashahada katika fani ya Umeme (Ordinary Diploma in Electrical Engineering).
ii. Umri usiozidi miaka 30 ifikapo mwezi wa Agosti 2018.
iii. Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

3. FUNDI SANIFU (ARTISAN) Nafasi – 1
Sifa za Muombaji
i. Awe amehitimu na kupata cheti cha elimu ya Sekondari (Form II or Form IV).
ii. Awe amehitimu na kupata cheti cha VETA.
iii. Umri usiozidi miaka 30 ifikapo Agosti 2018.

4. DEREVA (DRIVER) Nafasi – 2
Sifa za Muombaji
i. Awe amehitimu na kupata cheti cha elimu ya Sekondari (Form II or Form IV).
ii. Awe na leseni hai ya udereva.
iii. Umri usiozidi miaka 30 ifikapo Agosti 2018.
iv. Ujuzi wa ufundi gari ni sifa ya ziada.

5. MTUNZA GHALA (STORE KEEPER) Nafasi – 1
Sifa za Muombaji
i. Awe amehitimu na kupata Stashahada katika fani ya manunuzi na ugavi (Ordinary Diploma in Procurement and Logistic Management/ Material Management).
ii. Umri usiozidi miaka 40 ifikapo Agosti 2018.
iii. Awe na ujuzi wa kutumia kompyuta.

PEMBA

1. FUNDI SANIFU (ARTISAN) Nafasi – 1

Sifa za Muombaji
i. Awe amehitimu na kupata cheti cha elimu ya Sekondari (Form II or Form IV).
ii. Awe amehitimu na kupata cheti cha VETA.
iii. Umri usiozidi miaka 30 ifikapo Agosti, 2018.

Jinsi ya kutuma maombi.
Muombaji anatakiwa kuandika barua ya maombi akiambatanisha na vitu vifuatavyo:
i. Barua ya sheha wa shehia anayoishi muombaji.
ii. Vivuli (photocopy) vya vyeti vya kumalizia masomo, cheti cha kuzaliwa, kitambulisho cha mzanzibari na leseni kwa atakaeomba nafasi ya dereva.
iii. Maelezo binafsi (Curriculum Vitae) ya muombaji.
iv. Kila muombaji anatakiwa kuainisha juu ya bahasha nafasi anayoomba.
Maombi yanaweza kutumwa kwa lugha ya Kiswahili au Kiingereza.

Mazingatio;

Muombaji anasisitizwa kuandika namba yake ya simu na namba ya mtu wake wa karibu katika barua ya maombi kwa mawasiliano.

Maombi yote lazima yatumwe kwa njia ya Posta kupitia anuani;

Meneja Mkuu,
Shirika la Umeme,
S.L.P 235,
Zanzibar.

Tarehe ya mwisho ya kutuma maombi ni 13/Julai/ 2018.