Tahadhari kwa wenye kuweka mabango ya biashara Zanzibar

Mkuu wa Kitengo cha Matangazo Baraza la Manispaa Wilaya ya Mjini Amina Amour Yussuf amewataka wafanyabiashara wanaoweka mabango njiani kutangaza biashara zao wafuate masharti ya uwekaji wa mabango ili kuweza kufikia malengo yaliyokusudiwa na Serikali.

Bi. Amina Amour Yussuf amesema hatua ya kuondoa mabango ya wafanyabiashara ambao wamekiuka utaratibu uliowekwa na baraza si nzuri hivyo ni vyema wafanyabiashara wakazingatia masharti kwa maslahi yao binafsi na taifa kwa ujumla.

Amesema miongoni mwa masharti ya uwekaji wa mabango  ni kuzingatia upana na urefu wa eneo bango linapoekwa sambamba na kuchagua eneo stahili ili kuepusha madhara kwa jamii.

Rauhiya Mussa Shaaban.