Bausi asikitishwa na Mrajisi wa vyama vya michezo

Aliyekuwa kocha mkuu wa Timu ya Taifa ya Zanzibar na mchezaji wa zamani wa Zanzibar Heroes Salum Bausi amesikitishwa na kauli ya mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar kwa kutaka ZFA kufanya uchaguzi mdogo wakati katiba ya ZFA ina mapungufu makubwa sana.

Bausi amesema mrajisi mwenyewe amekiri katiba ya ZFA inamapungufu na yeye anataka uchaguzi mdogo ufanyike kwa katiba ile inaweza kusababisha kufanya waliotangaza nia ya kugombea wajitoe kwenye uchaguzi huo mdogo.

“Ingekuwa vizuri tungetafuta katiba ya CAF inayofatwa na vyama vyote vya michezo Afrika itengenezwe katiba watu wafanye uchaguzi kwa katiba ile hatuwezi kuingia kwenye uchaguzi sisi watu wa mpira” Alisema Bausi.

Hata hivyo Bausi amesikitishwa na kitendo cha kamati ya Uchaguzi kwa kufanya kikao na kujadili namna ya kufanya uchaguzi mdogo wiki iliyopita Bausi alidai kuwa kamati ya uchaguzi imeteuliwa vipi wakati sasa ZFA Raisi hayupo mwenye mamlaka ya kuteuwa kamati ya uchaguzi.

Bausi amedai endapo atakapopewa nafasi ya kuongoza ZFA ni atarejesha mpira wa Zanzibar katika kiwango kikubwa na ametaka mrajisi kuhakikisha suala la katiba linafanyiwa marekebisho suala la Katiba kwa kuwa hata ZFA ikifanya uchaguzi kiongozi hata toka nje ya ZFA kwa mujibu wa kanuni ya katiba hiyo ya sasa ya ZFA.

Bausi ni miongoni mwa wadau wa mpira wa miguu Zanzibar waliotangaza nia ya kuwania nafasi ya Urasi wa ZFA kwa muda mrefu ila katiba sasa haipi nafasi mtu kutoka nje ya ZFA kuwania nafasi ya ungozi wa juu wa ZFA mpaka ukuwemo kwenye kamati tendaji ya chama hicho.

Zanzibar24 ilimtafuta mrajisi wa vyama vya michezo Zanzibar Suleiman Pandu Kweleza huko ofisini kwake Baraza la Michezo Zanzibar Mwanakwerekwe kutaka ufafanuzi wa suala hili mrajisi amekiri mapungufu makubwa kwenye katiba hiyo ya sasa ya ZFA.

Aidha mrajisi amefafanua suala la katiba haliko chini yake bali katiba ya sasa imeelekeza utaratibu wa kuwapata viongozi watakao jaza nafasi hizo ni uchaguzi mdogo au kamati tendaji kuteuwa mtu atakaye beba dhamana ya kujaza nafasi hizi.

“Haya masuala ya ZFA yapo wazi lazima nafasi zijazwe isifike siku 60 uchaguzi mdogo lazima ufanywe kuhusu masuala ya katiba mimi nimeshaelekeza katiba irekebishwe ina mapungufu” Alisema Mrajisi.

Kuhusu Kamati ya Uchaguzi mrajisi Kweleza amesema kamati hiyo kwa mujibu wa katiba yao haijafafanua suala la kamati ya uchaguzi inamaliza kazi lini kwa hivyo siwezi kulitolea majibu.