Chadema watoa ufafanuzi juu ya Uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimetolea ufafanuzi juu ya uchaguzi mdogo wa jimbo la Buyungu mkoani Kigoma.

Tayari tume ya uchaguzi NEC imeshatangaza tarehe ya uchaguzi kwenye jimbo hilo ambalo lilikua chini ya mbunge wao Kasuku Bilago ambaye alifariki Dunia.

Chadema imemteua Eliya Michael kuwa mgombea wao na tayari ameshaanza kujaza fomu.

Akizungumza na wandishi wa habari Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Vicent Mashinji amesema tayari wameshaanza kufanyiwa figisu figusu na tume ya uchaguzi kwenye kata tano kati ya 79 ambazo nazo pia zitaingia kwenye uchaguzi.

 “Ukisoma katiba ya Nchi yetu inazuia wanachama wa vyama vya siasa kuwa watumishi wa Serikali, sasa tuna mzee wetu Mapuri ambaye kila mtu anafahamu aliwahi kuwa Katibu Muenezi wa CCM kwa miaka mingi.

” Tunaomba mkemee hizi vurugu za uchaguzi ambazo zinaendelea, mgombea wetu huko Kilosa amevamiwa na watu wasiojulikana na kumnyang’anya fomu zake za uchaguzi, viongozi wetu kule Tunduma wamekamatwa na kuwekwa ndani, hii hali isipokemewa itavuruga amani” amesema Dk Mashinji.

Dk Mashinji amezungumzia ushiriki wao wa Uchaguzi,” Lazima tukubaliane kuwa Viongozi lazima watoke ndani yetu, Sheria za Uchaguzi ni mbovu na hatuwezi kujificha kwenye kichaka cha Uongozi kwa kutoshiriki, muhimu ni kuwachagua Viongozi bora ili wakachague, pamoja na ubovu wa NEC lakini bado kuna eneo ambalo wananchi wamesimama kidete”,

kuhusu makubaliano yao na Chama cha ACT Wazalendo juu ya kusimamisha Mgombea mmoja, Dk Mashinji amesema Leo kuna kikao kinafanyika na baada ya hapo watatangaza nini kilichoamuliwa.