Cloud kuinua wasanii wa Zanzibar kupitia Tamthilia

Msanii wa filamu mzaliwa wa visiwani hapa Zanzibar Issa Mussa Khamis (CLOUD) anatarajia kutoa tamthilia mpya iliyosheheni wasanii kutoka Zanzibar kwa lengo la kukuza sanaa ya filamu Zanzibar.

Akizugumza na Zanzibar24 katika shamra shamra za tamasha la kimataifa la filamu Zanzibar Issa Mussa amesema series hiyo itakayoitwa” upande wa kanga “itaweza kutafsiri dhana ya wasanii wa Zanzibar kuwa nao wanaweza kufika mbali kama wataaumua kujituma zaidi hususan wasanii wachanga kwenye filamu.

Aidha amezugumzia tamasha hilo kwa kusema linaonekana ni tamasha zuri na linalipa heshima Zanzibar licha ya kuwa tamasha hilo kwa sasa lipo kipindi ambacho kombe la dunia linachezwa hali ya watu inakuwa ndogo sana kwenye shamra shamra hizo.

“Tupo kuisadia na kuitangaza filamu za Zanzibar na Tanzania kwa ujumla licha ya changamoto zinazoikabili filamu Zanzibar, upande Kanga itajibu hoja za wale wanao beza sanaa ya Zanzibar “Alisema Mussa.

Amemalizia na kutoa wito kwa wasanii wa Zanzibar kundelea kufanya kazi zao sanaa ni kazi kama kazi nyengine hivyo vijana wandelee kujituma zaidi.