Picha 6: Hali ilivyokuwa nchini Croatia baada ya timu yao kuifunga England Kombe la Dunia

Mashabiki wa Croatia walisherehekea usiku kucha baada ya taifa lao kuwaondoa England kutoka kwenye michuano ya Kombe la Dunia Urusi na kufuzu kwenda fainali kwa mara yao ya kwanza kabisa

Croatia walipata ushindi wa 2-1 baada ya mechi kumalizika sare ya 1-1 muda wa ziada.

Mashabiki walijaza uwanja ulio katikati mwa mji mkuu wa Croatia wa Zagreb wakiimba na kupeperusha bendera za taifa hilo. Baadhi walijitumbukiza hadi kwenye chemchemi za maji zinazopamba uwanja huo.

Mabao yalivyofungwa

Kieran Trippier dakika ya 5 Croatia 0-1 England

Ivan Perisic dakika ya 68 Croatia 1-1 England

Mario Mandzukic dakika ya 109 Croatia 2-1 England

Presentational white space

Croatia ni taifa la watu milioni nne hivi na ni moja ya mataifa yenye idadi ndogo sana ya watu kuwahi kufika fainali Kombe la Dunia.

Watakutana na Ufaransa katika uwanja wa Luzhniki mjini Moscow Jumapili kwa fainali saa tatu usiku saa za Afrika Mashariki ambapo England watakutana na Ubelgiji mechi ya kuamua atakayemaliza nafasi ya tatu, mechi ambayo itachezewa mjini St Petersburg.

 

Croatia's supporters celebrate a goal as they watch Croatia -V-England at the main square in Zagreb
Mashabiki wakisherehekea Zagreb

Croatia supporters celebrate the second goal as they watch on a giant screen the Russia 2018 World Cup semi-final football match between Croatia and England, at the main square in Zagreb
Mashabiki wengi walijitokeza Zagreb

Croatia's fans celebrate in Zagreb after Croatia beat England in semi-final of the 2018 World Cup
Mashabiki wakicheza kwenye maji kusherehekea katikati mwa mji wao mkuu Zagreb

Croatia President Kolinda Grabar-Kitarovic (L) offering a Croatia national football team jersey to British Prime minister Theresa May (R) at the NATO headquarters in Brussels
Rais wa Croatia Kolinda Grabar-Kitarovic (kushoto) alimpa waziri Mkuu wa Uingereza Theresa May jezi ya taifa hilo wakati wa mkutano mkuu wa Nato mjini Brussels, Ubelgiji

Croatia's midfielder Luka Modric (C) and Croatia's forward Mario Mandzukic (R) celebrate after winning the Russia 2018 World Cup semi-final football match between Croatia and England at the Luzhniki Stadium in Moscow on 11 July 2018.
Kiongo wa kati wa Croatia Luka Modric (kati) akiwa na Mario Mandzukic (kulia) wakisherehekea Luzhiniki, Moscow

A picture of Croatia fan Daniel holding a pint of beer and smiling
Shabiki huyu kwa jina Daniel alisherehekea kwa kinywaji, na aliambia BBC kwamba “ushindi huo ni mkubwa mno” kwa taifa hilo ndogo