Mtengezaji filamu ujerumani aja na filamu ya ukeketaji ZIFF

Ukeketaji ni moja ya changamoto zinazozikumba jamii nyingi za Tanzania mtengezaji filamu kutoka ujerumani Rechor Gil ameona haja ya kutengeneza filamu inayo husu masuala hayo kutokana na maisha ya kweli ya jamii hizo.

Akizugumza na wandishi wa Habari huko Hoteli ya African House mkoa wa mjini Magharib Unguja  katika muendelezo wa tamasha la Taifa la Filamu Zanzibar amesema suala la ukeketaji bado linawathiri wasichana wengi na kuamua kutengeneza filamu hiyo yenye maisha halisi ya ukeketaji Tanzania.

Aidha amesema filamu hiyo aliopa jina la “In the Name of Your Daughter” inatarajiawa kuonyeshwa karibia mikoa yote na kusambazwa duniani ili kupinga masuala ya udhalilishaji wa kinjisia unaoendelea hususan katika jamii za Afrika.

Rose Makole na Neema Chacha ni wasichana waliowakimbia familia zao kutokana na musuala ya ukeketaji wakiwa wadogo kutokana na kupata elimu ya ukeketaji wakiwa mashuleni .

Aidha wamesema Kwa pamoja walikimbia familia zao kwa hofu na kuhifadhiwa nyumba salama ambayo huwapokea watoto waliofanyiwa ukeketaji katika familia zao iliyopo chini ya dawati la Jinsia na watoto Tanzania.

Robi mlezi mkuu wa kituo hicho cha kituo salama kilichopo wilayani Serengeti na Butiama wamenzisha vituo hivyo baada ya kuona watoto wanao takiwa wanafanyiwa ukeketaji wanahitaji kulindwa lakini bado imekuwa changamoto sana.

“Natumai tatizo hili iko siku litakwisha na tayari linaendelea kwisha kidogo kidogo jamii zetu tayari zishaelimika na tunaendelea na elimu hii iko siku wazazi wa hawa watakuja kuwachukua watoto wao” Alimalizia Robi.

Filamu hiyo iliyotengenezwa kwenye mazingira halisi imesharikisha watoto hao ili kusambaza elimu kwa jamii ambayo bado haijaelimika bado kuhusiana na madhara ya ukeketaji kwa jamii za Afrika.