Sheria ya maadili kwa viongozi wa umma nchini bado ni changamoto 

Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, Jaji Mstaafu Harold Nsekela, amesema asilimia moja pekee ya wanawake katika ngazi ya vijiji na mitaa ndio wanaofahamu sheria ya maadili kwa viongozi wa umma.

Jaji Mstaafu Harold Nsekela ameyasema   hayo jijini Dar es Salaam wakati wa ufunguzi wa semina ya kuwajengea uwezo madiwani na wakuu wa idara kutoka Wilaya zote za jiji hilo.

Jaji Mstaafu Nsekela amebainisha katika utafiti uliofanywa na sekretarieti hiyo mwaka 2015 kwa lengo la kukuza uelewa wa wananchi kuhusu majukumu .

Sekretarieti kuandaa mafunzo haya katika mikoa inayotekeleza mradi huo ambayo ni Mtwata, Morogoro, Iringa, Dodoma na kuijumuisha Dar es Salaam kutokana na umuhimu wake.

Aidha amewataka viongozi hao kutumia mafunzo watakayoyapata kuhamasisha na kuwaelimisha wanawake wengine katika ngazi na kata na mitaa ili kuwawezesha kuwa na ujasiri wa kutoa taarifa kwa mamlaka husika kuona ukiukwaji wa maadili unaofanywa na viongozi wa umma.

Amesema moja ya misingi ya demokrasia ni kuwa na Serikali inayowajibika kwa wananchi na yenye viongozi wanaowatumikia wananchi kwa uadilifu.

Amesema Wananchi wanategemea kwamba viongozi watatumia nafasi zao za uongozi kuwaletea maendeleo na si vinginevyo. Sote tunafahamu kwamba uongozi ni dhamana, kiongozi yeyote awe wa kuchaguliwa ama wa kuteuliwa, amekabidhiwa madaraka na wananchi.

Aliongeza kuwa uadilifu ni sharti ujengwe ndani ya jamii ili uwe sehemu ya utamaduni wa nchi na kwamba sheria ya maadili ya viongozi wa umma, kanuni za serikali za mitaa na vyombo vya kusimamia utawala bora pekee haviwezi kukuza na kusimamia maadili.