Singida United yanasa saini ya ‘Fei Toto’ kutoka JKU

Klabu ya Singida United imefanikiwa kumsajili, Kiungo mahiri wa JKU na timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes pamoja na Taifa Stars Feisal Salum Abdalah maarufu kama ‘Fei Toto’ kwa kandarasi ya miaka mitatu.

Meneja wa Singida United, Hemedi Selemani Morocco amefanikiwa kumpata kijana huyo kwa kushirikiana na JKU na kuridhia gharama zilizo hitajika.

Kiungo huyo mahiri wa JKU na timu ya taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes pamoja na Taifa Stars, Fesal Salum “Fei Toto” alifanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora kupitia michuano ya Mapinduzi Cup.