Waziri wa habari Zanzibar afanya uteuzi

WAZIRI wa Habari, Utalii na Mambo ya Kale Mhe. Mahmoud Thabit Kombo, leo Julai 12, 2018 amemteua ND. OMAR SAID AMEIR (KIMIMBI), kuwa Mrajis wa Tume ya Utangazaji Zanzibar.

Mhe. Waziri amefanya uteuzi huo kwa mujibu wa uwezo aliopewa chini ya kifungu cha 9 (2), cha Sheria Namba 7 ya Tume ya Utangazaji Zanzibar ya mwaka 1997.

Uteuzi huo umeanza rasmi tarehe 11 Julai, 2018.

Kabla ya uteuzi huo, ND. OMAR SAID AMEIR alikuwa mwandishi wa habari mwandamizi katika Shirika la Magazeti ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

IMETOLEWA NA WIZARA YA HABARI, UTALII NA MAMBO YA KALE.