Mtoto auawa kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali Donge Kaskazini Unguja

Mtoto mwenye umri wa miaka 17 ameuawa usiku wa kuamkia leo Julai 13, 2018 kwa kuchomwa na kitu chenye ncha kali huko Donge Mtambile mkoa wa Kaskazini Unguja.

Kwa mujibu wa ndugu wa karibu wa marehemu wamesema Marehemu alikuwa mwanafunzi wa kidato cha pili katika skuli ya Donge Muwanda.

Akithibitisha kutokea kwa mauaji hayo Kamanda wa Polisi mkoa huo Haji Abdallah Haji amesema “Ni kweli jana majira ya saa 4 usiku imeletwa taarifa kijana Miraji Shaame Haji miaka 17 wa Donge Mtambile amejeruhiwa kwa kitu chenye ncha kali, Ameongeza kuwa “alikimbizwa hospitali ya Mnazimmoja ambako alifariki dunia”.

Amesema Jeshi la Polisi linaendelea na upelelezi kujua chanzo cha tukio hilo ambapo kwasasa wanawashikiliwa watu wawili wenye umri kati ya miaka 16-17 wanaotuhumiwa kuhusika na tukio hilo.

Mwili wa marehemu tayari umeshakabidhiwa kwa ndugu na jamaa zake kwaajili ya taratibu za mazishi.