Necta yawafutia matokeo watahiniwa wanane kwa sababu hizi….

Baraza la taifa (Necta) limefuta matokeo ya watahiniwa wanane, waliofanya mtihani wa kidato cha sita kutokana na udanganyifu.

Akitangaza matokeo hayo leo Julai 13, Katibu Mtendaji wa Necta, Charles Msonde amesema watahaniwa hao walibainika kufanya udanganyifu wakati wa mtihani

Kati ya watahiniwa hao wanane waliofutiwa matokeo, wanne ni wa shule na wanne ni wa kujitegemea.

Hata hivyo baraza limezipongeza kamati za shule kwa kusimamia vizuri mitihani hiyo na hivyo kuzuia udanganyifu kwa kiasi kikubwa.

“Baraza pia linawapongeza watahiniwa wote waliofanya mitihani kwa kutofanya udanganyifu,” amesema

Bonyeza hapa kutazama matokeo ya kidato cha sita