Wizara ya Afya Zanzibar yapokea msaada wa Dawa na Vifaa Tiba kutoka WHO

BAADHI ya Dawa na Vifaa Tiba vilivyotolewa na Shirika la Afya Ulimwenguni (WHO)  kwa Wizara ya Afya Zanzibar.

 

MWAKILISHI wa Shirika la Afya Ulimwenguni Tanzania (WHO) Dkt. Adiele Onyeze akizungumza katika hafla ya Makabidhiano ya  Dawa na Vifaa Tiba vilivyotolewa na Shirika la Afya Duniani  kwa Wizara ya Afya Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Ngalawa Bububu Mjini Zanzibar.

 

NAIBU Waziri wa Afya Zanzibar Harus Said Suleiman pamoja na Mwakilishi wa  WHO Tanzania Dkt. Adiele Onyeze wakitiliana saini makabidhiano ya Dawa na Vifaa Tiba kwaajili ya Wizara ya Afya Zanzibar katika hafla iliyofanyika katika Hoteli ya Ngalawa Bububu  Zanzibar.

 

NAIBU Waziri wa Afya Zanzibar Harus Said Suleiman akibadilishana hati za makabidhiano ya Dawa na Vifaa Tiba na Mwakilishi wa WHO Tanzania Dkt. Adiele Onyeze katika hafla iliyofanyika Hoteli ya Ngalawa Bububu Zanzibar.

Picha na Abdalla Omar  Maelezo  – Zanzibar.