Aliyewahi kuwa Mbunge wa Kasulu Mjini(NCCR) na kuhamia ACT-Wazalendo, Moses Machali ahamia CCM kumuunga mkono Rais Magufuli. Amfananisha na Sokoine, Nyerere.

Amesema Serikali ya Awamu ya Tano imeonyesha njia katika mambo mengi na inastahili kuungwa mkono.

Amesema hata kelele wanazopiga baadhi ya watu kwamba maisha yamekuwa magumu kwa sababu ya Magufuli ni propaganda tu kwa sababu hakuna uhusiano wa maisha magumu na suala la KUDHIBITI wapiga dili wa fedha na mali za umma.